Wanawake wa Urusi Wapigwa Marufuku Kutofanya Mapenzi na Raia wa Kigeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wanawake wa Urusi watakiwa kutofanya mapenzi na raia wa Kigeni
Mbunge mmoja nchini Urusi anasema kuwa wanawake hawafai kufanya mapenzi na wageni wakati wa kombe la dunia huku akionya kuhusu watoto wanaozaliwa kutoka rangi tofauti.

Tamara Plentyova mkuu wa familia , wanawake na kamati ya maswala ya watoto , alisema kuwa hata iwapo uhusiano huo utasababisha kufanyika kwa harusi , wanawake au watoto wao watachukuliwa na nwanamume huyo ambaye atakuwa raia wa kigeni.

''Hata wakiolewa, watawachukua, halafu atashindwa namna ya kurudi'' , bi Pletnyova alisema katika kituo cha Govorit Moskva.

"Baadaye watakuja kwangu , wasichana wakilia kwamba watoto wao wamechukuliwa''.

Alisema kuwa wanawake waliopata watoto na raia wa kigeni wakati wa michezo ya Olimpiki ya 1980 mjini Moscow walisalia kuwa wanawake wasio na wanaume.

''Ni vyema iwapo ni mtu wa rangi inayofanana na yako lakini iwapo ni mtu wa rangi tofauti basi kunakuwa na shinda''.

''Ni muhimu kuwa na watoto wetu'', alisema bi Pletnyova.

Warusi wenye rangi tofauti walikuwa wakiitwa 'watoto wa Olimpiki' ama 'watoto wa sherehe' baada ya Muungano wa Sovieti kuwaalika Waafrika, watu wa mashariki ya kati na raia wa Marekani kusini.

Warusi wenye ngozi nyeusi hadi leo hukabiliwa na maswali mengi ya ubaguzi wa rangi katika taifa ambapo chini ya asilimia moja ya idadi ya watu ni watu weusi.

Zaidi ya watalii milioni moja wa kigeni wanatarajiwa kuhudhuria kombe la dunia, swala linalozua wasiwasi kuhusu ubaguzi wa rangi na wapenzi wa jinsia moja hususan wakati ambapo wanachama wenye msimamo mkali wa Cossack watazuru mataifa yanayoandaa dimba hilo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad