Ushauri wa Bure Kwa 'Rockstar' Ali Kiba, Kaka Siku Hazigandi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Awali ya yote naomba nitangaze "mahaba" yangu (decralation of interest) kwa mwanamuziki nyota nchini Ali Kiba, kwamba mimi ni mshabiki wako wa kutupwa. una sauti nzuri, una kipaji cha hali ya juu, una jina Tanzania, Afika Mashariki, Afrika na duniani kote. Hiyo haina ubishi. Hivyo nisemayo hapa hayahusiani na hujuma ama ushabiki wa aina yoyote. Bali ni hasira tu. Naomba unisamehe kama nitakukwaza. Cos I feel you buddy!

Nimesukumwa kusema haya baada ya kuperuzi mtandaoni na kukuta picha yako hii Ali Kiba ukiwa na Diamond. Nikasema woow! (japo body language haisemi hivyo) na kufurahi kwamba kumbe mmeshawahi kukutana. Nilifurahi sana.

Hata hivyo, furaha yangu hiyo ikawa fupi (short lived) nikivuta kumbukumbu ya mambo kibao katika fani yenu nyie wawili (ninayoifananisha kama Yanga na Simba vile - najua Diamond ni Simba kindakindaki, hivyo bila shaka we Ali ni wa mitaa ya Twiga na Jangwani - aka Kaunda Stadium) maana mpo kama hampo vile.

Kama hizo kumbukumbu zangu haziko mbumbumbu kama nilivyo, hadi naandika haya nadhani kama ni mechi mabao ni 6-0, na Diamond ndiye mshindi. Yaani kila niamkapo nategemea Ali unafanya mashambulizi dhidi ya mpinzani wako Diamond, nakuta patupu. Yaani wewe umekuwa adimu mno katika tasnia wakati mwenzako kila uchao anakuja na ngoma mpya, tena sio ngoma tu bali NGOMA KALI.

Kumbukumbu zangu mbumbumbu zinaniambia kwamba umewahi kunukuliwa ukisema ukimya huamsha hisia. Yaani unajifanya Michael Jackson kwa kutoa kibao kimoja baada ya kingine kwa msimu, na kwamba kutoa vibao kila mara sio dili. Kaka Ali nakupa point blank kwamba hapo umenoa. Yaani ukisubiri siku kibao ndio utoe kitu kwa kujiamini utakubalika kwa mgongo wa kuwa wewe ni "Rockstar" kaa ukijua unakosea. Unatukosea mashabiki wako KAKA!! Tunahitaji vitu kila mara ili tujue ukio hai na fiti. Hayo mambo ya kuiga kina Beyonce na Jay Z (yaani hata kwenye insta huja-follow mtu kwa staili yao hao ni ujuha). Siku hazigandi KAKA ALI. Umwinyi, Ujuaji na kujiona uko juu vitakuzamisha! Piga kazi baba! Sie mashabiki zako tunategemea ukija kwenye show uje na jioya sio na ma "dusherere" na kubweka kama mbweha kila uchao.

Ona mwenzio Diamond anavyowika. Yeye ni mega star kama wewe lakini hategemei kubebwa na historia ya "ALIKUWA" (has been) kwa kutegemea nyota zilipendwa. Ona sasa ngoma yako latest ya "Mvumo wa Radi" ilivyododa. Hiyo ni bonge moja la ngoma lakini imepitwa na wakati. Najua una producer kabambe nchini (Man Water) lakini maudhui ya ngoma hiyo ni two years old! Wakati mwenzio Diamond kaibuka na vitu vya moto kibao ikiwemo hii ya "Baila" aliyo-shoot London, wakati wewe una ngoma kali kuliko hiyo/hizo ambazo hutaki kuzitoa eti kisa hutaki kumwaga lazi kila mara, Ujuha huo Ali Kiba! AMKA!

Sie mashabiki wako tumeshachoka na masebene yako ya "Dusherere" na tunataka utoke upya kila mara udhihirishe u "Rockstar" wako bhana! Hayo mapicha kwenye insta ya kuonesha fashion za mkeo na kujirusha na meneja wako Seven havisaidii kitu. Unatakiwa baada ya ndoa yako hata wakwezo wa Mombasa wajue kweli wana mkwe Star na sio bishoo wa kuishia kwenye Insta kuonesha leo umeenda wapi na mkeo kavaa nini. Huo ni UJUHA kaka. Piga kazi utuliwaze mashabiki zako!!!!!

Naomba nimalizie kwa kukupa ushauri wa bure: Acha nyodo, siku hazigandi, piga kazi, lete mambo mapya ili tujue kuwa naam! tunayemshabikia ana uwezo. Sio kuuza sura na makanzu yako (yanaboa!) huku ukitembelea nyota yako zilipendwa. Yaani unatakiwa utengeneze vitu na kuvimwaga hapo hapo. Kama ushauri huu utaupuuza basi jiandae kuanguka maana kila mtu nchini na nje anakuona wewe ni mtu wa makidai, mtu wa nyodo, usieambilika na juu ya yote unadhani yale ya kale yaliyokupaisha yatadumu. Acha ujuha wa Kiswahili, PIGA KAZI ionekane. Kazi mpya kaka tunataka kila uchao.

By Tarishi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad