Bobi Wine Awaandikia Barua Yenye Ujumbe Mzito Watoto Wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bobi Wine Awaandikia Barua Yenye Ujumbe Mzito Watoto Wake
Leo Agosti 24, 2018 nakusogezea stori ambayo imezidi kuteka hisia za Watu wengi katika ukanda wa Afrika Mashariki na stori hii inamhusu Mbunge Bobi Wine wa nchini Uganda ambapo baada ya jana Agosti 23 kuondolewa mashtaka na Mahakama ya Kijeshi na kushtakiwa tena katika mahakama ya Kiraia kwa tuhuma za uhaini, leo asubuhi zimesambaa barua mbili mtandaoni ambazo zinadaiwa kuandikwa na Mbunge huyo kwenda kwa Watoto wake.

Katika barua hizo Mbunge huyo amewaelezea Watoto wake sababu ya kutorudi nyumbani kama ambavyo aliwaahidi.

“Naandika barua hii kutoka gereza la Kijeshi Makindye, samahani sana Watoto wangu sitaweza kurudi nyumbani kama nilivyowaahidi kwa sababu nimepatwa na matatizo ambayo Mama yenu atawaeleza kwa kirefu zaidi lakini mkiendelea kuniombea nitawahi kurudi nyumbani ili tuwe pamoja”, ameandika Bobi wine.

Mbunge huyo pia katika moja ya barua hizo amewataka Watoto wake kuwa shupavu na kumjali sana Mama yao katika kipindi ambacho yeye hayupo.

Bado hakuna chanzo cha kuaminika kilichothibitisha kama barua hizo ziliandikwa kweli na Mbunge huyo.

Mbunge Bobi Wine atafikishwa tena katika Mahakama ya Gulu nchini humo Agosti 30 kujibu tuhuma za uhaini zinazomkabili. 

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad