IGP Sirro Amteua Kamanda Ahmed Msangi Kuwa Mkuu wa Kitengo cha Makosa Dhidi ya Binadamu Dar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

IGP Siro Amteua Kamanda Ahmed Msangi Kuwa Mkuu wa Kitengo cha Makosa Dhidi ya Binadamu Dar
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro,  amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza na mkoa wa Pwani.



Katika mabadiliko hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, (DCP), Ahmed Msangi amekuwa Mkuu wa Kitengo cha Makosa Dhidi ya Binadamu, Makao Makuu ya Upelelezi jijini Dar es salaam, huku nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Jonathan Shana,  ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani.



Aidha, nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Wankyo Nyigesa ambaye alikuwa Mkuu wa Oparesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imesema  mabadiliko hayo ni kawaida  ndani ya jeshi la Polisi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad