Wanaotorosha Madini ya Tanzanite Kukiona Chamoto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wanaotorosha Madini ya TanzaniteKukiona Chamoto
Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema Serikali itaaendelea kusimamia  ulinzi  na kudhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite na watakaokwenda  kinyume na matakwa ya Sheria, kiama chao  kinakuja.

Waziri Kairuki aliyasema hayo tarehe 1 Agosti wakati wa ziara yake mkoani Manyara wakati alipotembelea migodi mbalimbali ya madini  ya tanzanite ndani ya ukuta wa Mirerani.

Alisema ziara hiyo ililenga kuangalia suala zima la ulinzi katika ukuta unaozunguka migodi  ya tanzanite, shughuli za uchimbaji madini  mengine zinavyofanyika na kuangalia namna uzalishaji wa madini ya tanzanite  unavyoendelea katika migodi husika.

Kairuki aliongeza kuwa, ziara hiyo ililenga  kuangalia namna Sheria ya Madini inavyotekelezwa, masuala ya Mikataba ya watumishi katika migodi  na namna migodi husika inavyolipa  kodi  mbalimbali za Serikali  yakiwemo masuala ya usalama sehemu za kazi na  wafanyakazi kwa ujumla.

“Utoroshaji madini hausaidii, fedha ni za haraka lakini zinawaadhibu watanzania walio wengi kwa kuwa, fedha hizo hizo zingeweza kutumika katika miradi mingine ya maendeleo. Hivyo, kila mtanzania awe mlizi wa mwenzake,” alisema Kairuki.

Awali, akizungumza  katika eneo Lemshuku kunakofanyika shughuli za uchimbaji wa madini ya Green Garnet, waziri Kairuki alisema kuwa, serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika kuchangia pato la taifa kupitia shughuli za uchimbaji, hivyo akawaasa wachimbaji nchini kufuata Sheria, kanuni na taratibu ili kufanya shughuli halali ikiwemo kulipa kodi stahiki.

Akizungmzia suala la ruzuku kwa wachimbaji wadogo, waziri Kairuki alisema hivi sasa serikali imesitisha kwa muda utoaji rukuzu kwa kuwa inaandaa utaratibu wa wazi na endelevu ambao utawezesha wachimbaji  na serikali kunufaika kupitia rasilimali madini.

Aliongeza kuwa, serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa shughuli za uchimbaji mdogo wa madini ikiwemo kuhakikisha kuwa inawawezesha wachimbaji kutoka uchimbaji mdogo kwenda katika uchimbaji wa kati na kuongeza, “ tayari tumetenga maeneo zaidi ya 44 kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

Akitolea ufafanuzi suala la vibarua katika migodi ya madini, aliwataka wale wote wanaofanya vibarua katika maeneo hayo kuhakikisha kuwa, wanapata mikataba yao kabla ya kuanza kazi.

Kuhusu masuala ya utoaji leseni za uchimbaji madini, Waziri Kairuki  alisema   ndani ya kipindi cha wiki 2 Tume ya Madini itaanza kutoa leseni kwa waombaji waliokidhi vigezo na kuongeza kuwa, kwa wanaomiliki leseni bila kuziendeleza watanyang’nywa na hivyo akawaasa wamiliki wasiokuwa na uwezo wa kuendeleza maeneo yao kutoa tarifa ili waweze kuunganishwa na wenye uwezo wa kuwekeza waweze kushirikiana.

Pia, waziri Kairuki alihamasisha kuhusu uwekezaji katika mashine za kukata na kunga’risha madini ili kuwezesha shughuli hizo kufanyika nchini na kuongeza kuwa, kupitia Sheria Mpya ya Madini  hairuhusu yoyote kusafirisha madini ghafi nje ya nchi.

Kwa upande wake,  Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mlabwa, alisema  ni lazima Sheria, Kanuni na taratibu zizingatiwe wakati wa utekelezaji shughuli za uchimbaji madini na kuongeza kuwa, serikali inatambua mchango wa kila aina ya madini yanayopatikana nchini.

Naye, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Tumaini Magesa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto alisema kuwa, shughuli za uchimbaji katika eneo la Mirerani zinaendelea na hivyo serikali itaendelea kuboresha ulinzi na kuhakikisha kwamba unaimalika.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad