Mimi Ndio Mfalme wa huu Muziki Hakuna Anayeweza Kunipangia cha Kuongea- Afande Sele

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mimi Ndio Mfalme wa huu Muziki Hakuna Anayeweza Kunipangia cha Kuongea- Afande Sele
Mfalme wa Rhymes nchini Tanzania, Afande Sele amesema hakuna mtu ambaye anaweza kumpangia kitu cha kuongea, kwa madai yeye yupo kwa lengo la kuivusha nchi kutoka sehemu ya dhiki na kuipeleka sehemu nzuri.


Afande Sele ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii usiku wa leo Septemba 03, 2018, baada ya kusambaa sauti yake mitandaoni aliyokuwa akizungumzia sakata la Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally kuwa ameona mbali kuwazuia wasanii wa bongo fleva na filamu katika shughuli za kichama. Kwa madai wapo baadhi ya wasanii hao walikuwa wakiichafua CCM kutokana na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na picha za nusu utupu.

"Mimi ndio Mfalme wa huu muziki wa kizazi hiki, msitake kunipangia niongee hiki au hiki. Mimi naongea kile kinachostahiki chenye muelekeo wa kuitoa hii nchi kwenye dhiki na unafiki hata kama itanisababishia chuki au ikibidi kufariki, kwani hata nikikaa kimya miaka 80 sivuki", amesema Afande Sele.

Afande Sele ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa bongo fleva ambaye alijiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM), mnamo Machi 15, 2018 mbele ya Rais Dkt. Magufuli kwa lengo la kuunga mkono jitihada zake anazozifanya katika kupigania na kukiomba chama hicho kimpokee kama kijana wao.

Kwa upande mwingine, Afande Sele aliwahi kugombea Ubunge Jimbo la Morogoro Mjini mwaka 2015 kupitia chama cha ACT Wazalendo kabla ya kujivua uanachama na kusema kuwa hataki tena kujihusisha na siasa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad