Steve Nyerere Atoa Kali ya Mwaka "Nikifa Watoto Wangu Wasomeshwe na Ray"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Steve Nyerere Atoa Kali "Nikifa Watoto Wangu Wasomeshwe na Ray"
CHEKESHAJI maarufu Bongo, Steve Nyerere amesema ingawa watu wamekuwa wakimkashifu kwa roho yake ya kujitolea na kusimamia misiba ya mastaa mbalimbali, lakini hatakoma kusimamia kwani ni kitu anachokifanya kutoka moyoni na kwamba ikitokea amefariki basi watoto wake wasomeshwe na msanii mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’.

Akipiga stori mbili tatu na Star Showbiz, Steve alisema kitendo hicho cha kusimamia misiba kimeweza kwa namna moja au nyingine kumfanya pia awe karibu na watu wazito nchini ambao wanamuunga mkono kwenye kujitolea kwake.

“Sitaacha kusimamia misiba ng’o, wanaosema waache waseme watachoka. Ninasimamia misiba kwa sababu ninafahamu na mimi ipo siku nitaondoka na watu watasimamia msiba wangu. Niseme tu wazi hata kama nikiondoka leo nataka Vincent Kigosi ‘Ray’ asimamie na kuwasomesha wanangu,” alimaliza Steve bila kutoa sababu hasa iliyofanya achukue uamuzi wa kutangaza hilo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad