Mlivyofungwa na Cape Verde Nilishukuru sana sikutoa Dreamliner- Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mlivyofungwa na Cape Verde Nilishukuru sana sikutoa Dreamliner- Rais Magufuli
Rais John Magufuli amesema matokeo ya mchezo wa kufuzu AFCON 2019 kati ya Cape Verde na Taifa Stars uliopigwa mjini Praia yalimuumiza sana lakini alishukuru hakutoa ndege ya Dreamliner kwaajili ya kupeleka wachezaji.



Rais ameyasema hayo leo, mbele ya wachezaji wa Stars, viongozi wa TFF, Waziri Mwakyembe na Waziri wa Mambo ya Nje Augustine Mahiga alipowaalika Ikulu kwaajili ya mazungumzo na kupata chakula cha mchana.

"Nilitaka kwenye hatua za mwisho kwaajili ya kutoa ndege (Dreamliner) lakini dakika za mwisho nikaambiwa uwanja wa ndege ni mdogo cha ajabu nilipokuwa naangalia mchezo, kipindi cha kwanza tu tayari wamepigwa bao mbili, nikasema afadhali kiwanja cha ndege kilivyokuwa kidogo'', amesema Rais Magufuli.


Mbali na hilo Rais Magufuli amewataka viongozi wa TFF kutompangia kocha Emmanuel Amunike wachezaji wa kuwachezesha kwani yeye ndio anajua nani anastahili kucheza na nani hastahili.

Pai amewataka kutumia vizuri fedha zinazotolewa na wadau kwaajili ya kusaidia timu za taifa kitu ambacho kitasaidia kuwa na fedha nyingi kwaajili ya posho za wachezaji ambazo zitaongeza morali ya wachezaji.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mzee umesahau kusema hongera na jinsi ulivyofurahia ushindi wa vijana

    ReplyDelete

Top Post Ad