Saudi Arabia Yathibisha Mwandish wa Habari Khashoggi Alikufa Ddani ya Ubalozi wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Saudi Arabia Yathibisha Mwandish wa Habari Khashoggi Alikufa Ddani ya Ubalozi wake
Saudi Arabia imesema mwandishi wa habari Jamal Khashoggi alikufa baada ya kupigana kwenye ubalozi wake mdogo wa mjini Istanbul, Uturuki.Uchunguzi bado unaendelea na hadi sasa raia 18 wa Saudi wamekamatwa.



Taarifa ya vyombo vya habari vya serikali nchini Saudi Arabia imeongeza kusema kuwa mshauri wa mahakama ya Saudi Arabia, Saud al-Qahtani na naibu Mkuu wa idara ya upelelezi Ahmed Asiri wamefukuzwa kazi. Kabla ya Saudi Arabia kutoa taarifa hiyo mapema leo, rais wa Marekani Donald Trump alisema anaweza kuzingatia kuiwekea vikwazo Saudi Arabia lakini wakati huo huo amesisitiza umuhimu wa uhusiano wa nchi hizo mbili. Trump amesema maelezo yaliyotolewa na Saudi Arabia ni ya kuaminika.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la Saudi Arabia (SPA) mabishano kati ya Jamal Khashoggi na watu aliokutana nao kwenye ubalozi huo mdogo yaligeuka na kuanza kurushiana Makonde ugomvi ambao ulisababisha kifo chake. Hata hivyo Saudi Arabia haikutoa ushahidi wa kuunga mkono maelezo yake kuhusu hali halisi ilivyokua na haijulikani kama washirika wake wa Magharibi wataridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Saudi Arabia. Mkasa wa kutoweka mwandishi huyo wa habari ulisababisha kilio kutoka kwa jamii ya kimataifa na pia kuleta hali ya mvutano kati ya Saudia na nchi za magharibi. Uchunguzi bado unaendelea lakini hadi sasa raia 18 wa Saudi wamekamatwa.



Taarifa ya vyombo vya habari vya serikali nchini Saudi Arabia imeongeza kusema kuwa mshauri wa mahakama ya kifalme Saud al-Qahtani na naibu Mkuu wa idara ya upelelezi Ahmed Asiri wamefukuzwa kazi. Kabla ya Saudi Arabia kutoa taarifa hiyo mapema leo, rais wa Marekani Donald Trump alisema anaweza kuzingatia kuiwekea vikwazo Saudi Arabia lakini wakati huo huo amesisitiza umuhimu wa uhusiano wa nchi hizo mbili.

Vyombo vya habari vya serikali ya Uturuki vimekuwa vikidai mara kwa mara kwamba Khashoggi aliteswa na kuuuawa na kuchinjwa na kikosi cha makatili wa Saudi Arabia ndani ya ubalozi, lakini Uturuki bado haijafafanua maelezo kamili kuhusu uchunguzi wake.

Saudi Arabia hapo awali ilizikanusha tuhuma kwamba Khashoggi aliuawa katika ubalozi wake mdogo na kuzitaja tuhuma hizo kuwa hazina maana. Vyombo vya habari vya serikali ya Saudi Arabia pia vilipuuza madai kutoka kwa maofisa wa Uturuki kuwa kikosi cha Saudi “cha mauaji,” ikiwa ni pamoja na afisa mmoja kati ya washirika wa ndani wa mwana mfalme Mohammed bin Salman na mtaalam wa kuchunguza maiti  kilikwenda mapema na kumsubiri Khashoggi ndani ya ubalozi huo mdogo mjini Istanbul.



Muda mfupi kabla ya tangazo la Saudi Arabia, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Mfalme Salman walikubaliana kupitia njia ya simu kuendelea kushirikiana katika uchunguzi wa kutoweka kwa Khashoggi. Msemaji wa ikulu ya Marekani Sarah Huckabee Sanders amesema Marekani imesikitishwa na uthibitisho wa kifo cha Jamal Khashoggi, na amewatumia rambirambi familia yake, mchumba na marafiki zake.

Khashoggi, aliyekuwa mkosoaji mkuu wa sera ya mwana mfalme Mohammed bin Salman, alitoweka baada ya kuingia ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul mnamo tarehe 2 mwezi huu kwa ajili ya kupata hati ambayo ingelimwezesha kufunga ndoa na mchumba wake wa Kituruki.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad