Shamsa Ford Awatolea Povu Wanaosubiria Aachike

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shamsa Ford Awatolea Povu Wanaosubiria Aachike
STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford amesema kuwa, anashangaa kila akiposti chochote mtandaoni watu wanasema ameachika, jambo ambalo halina ukweli na wanaosubiri aachike, watasubiri sana.

Akizungunza na Risasi Jumamosi, Shamsa alisema kila akiweka ‘status’ kwenye ukurasa wake wa Instagram inayohusu ishu za kuachana, kuna wanaodhani inamhusu yeye, wakati huwa kuna ambao wamekuwa wakiomba ushauri na kwa sababu hawezi kumshauri kila mtu kwa wakati wake, huamua kuandika kwenye ukurasa wake.

“Unajua nilipoweka ‘status’ kila mtu alinihoji na wengine kunifuata ‘DM’ wakitaka kujua nini kimenikuta, niwaambie tu kwamba sitaachika mpaka Mungu atakapotutenganisha ingawa wapo wanaoniombea hilo kila siku,” alisema Shamsa.

Shamsa alitupia ‘status’ inayosomeka hivi: ‘Mapenzi au kumpenda mtu, kusikufanye uwe mtumwa… ukiona unampenda mtu halafu anakuchukulia poa achana naye. Maisha ya sasa hivi, siyo ya kujipendekeza au kulazimishana… mtu uwaze maisha magumu bado mapenzi yakusumbue? Acha ujinga na usikubali kuwa mtumwa… wewe funika sura fanya kama huoni..’
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad