Mambosasa: Waliomteka Mo Dewji Walikuwa Wanataka Fedha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mambosasa: Waliomteka Mo Dewji Walikuwa Wanataka FedhaWaliomteka Mohammed Dewji walitaka fedha na imeelezwa hiyo ndiyo ilikuwa nia yao. Dewji tayari amepatikana baada ya kuachiwa na watekaji hao.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema watekaji hao walikuwa wakimuuliza Mo Dewji kuhusiana na masuala ya fedha, naye akawaambia wampigie baba yake mzazi ingawa hawakufanya hivyo.


"Mo amesema watekaji hao walitaka fedha. Hata hivyo yeye aliwasisitiza kumpigia baba yake kwa kuwa yeye alikuwa nao pale," alisema.

Mo amerejea nyumba ikiwa ni siku ya tisa baada ya kutekwa na watu wasiojulikana Alhamis Oktoba 11 katika Hoteli ya Colessium iliyopo Masaki jijini Dar es salaam.


Ameungana na familia yake akiwa salama baada ya kupatikana usiku wa kuamkia leo kutokana na watekaji hao kumuachia wakitumia gari lilelile walilotumia kumteka.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad