Watoto wa Familia moja wachinjwa Kinyama Huko Bukoba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watoto wa Familia moja wachinjwa Kinyama Huko Bukoba
Watoto wawili wa familia moja wamechinjwa na miili yao kutupwa kichakani katika kijiji cha Mashule wilayani Bukoba Mkoa wa Kagera, ikiwa ni baada ya kupotea kwa siku moja.

Mkuu wa Wilaya hiyo,  Deodatus Kinawilo amethibitisha tukio hilo na kubainisha kuwa amewaagiza polisi kufanya uchunguzi na kuwakamata wahusika wa tukio hilo.

Amewataja watoto hao kuwa ni Auson Respikius (7) na Alistidia Respikius (5) walioondoka nyumbani Jumapili Oktoba 21 na miili yao kupatikana jana.

Baba wa watoto hao,  Respikius John amesema waliaga wanakwenda kucheza na wenzao, aliwaogesha na kuwaandalia nguo.

Amesema baada ya kucheza walirejea nyumbani jioni na kubadili nguo na kuondoka tena lakini hawakuonekana hadi miili yao ilipokutwa kichakani
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad