CHADEMA Kulipa Fidia Wananchi Waliobomolewa Nyumba zao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

CHADEMA Kulipa Fidia Wananchi Waliobomolewa Nyumba zao
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (CHADEMA) amewataka wananchi wa Ubungo kuhifadhi vyema nyaraka zao za maeneo waliyobomolewa na kwamba CHADEMA ikiingia madarakani watahakikisha wanawalipa fidia zao.

Kubenea ameyasema hayo jana  ikiwa ni siku moja kupita tangu Rais John Pombe Magufuli alipotamka hadharani kuwa wahanga waliobomolewa nyumba kuanzia maeneo ya Ubungo hawatalipwa fidia kwa kuwa walivunja sheria kwa kujenga kwenye hifadhi ya barabara.

Akizungumza jana na wanahabari, Kubenea amedai kushangazwa na kauli ya rais kwamba waliovunjiwa nyumba walijenga kwenye hifadhi ya barabara lakini serikali ndiyo iliyokuwa ikipokea kodi zao, kuwapatia hati za maeneo, kuwawekea maji na umeme huku wakijua hilo ni eneo la hifadhi.

"Naomba wananchi wa Ubungo, Kimara waliovunjiwa nyumba zao wahifadhi vizuri nyaraka zao. Mungu akipenda Sisi CHADEMA tukiingia madarakani tutalipa waathirika wote waliobomolewa kuanzia ubungo hadi Kibaha. Inawezekana siyo lazima CHADEMA waingie madarakani lakini anaweza akaja kiongozi mwingine akalipa. Hii inawezekana," alisema Kubenea.

Akiipigilia msumari kauli yake, Kubenea alisema kwamba, "Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika 1977, Serikali ya Mwl. Nyerere haikuipa kipaumbele kuwalipa wastaafu na hata seriakali ya Rais Mwinyi, ila serikali ya Mkapa yenyewe ililipa ikiwa ni baada ya miaka 30. Hivyo wanaweza wasipate wao malipo hayo lakini vizazi vyao vitakuja kunufaika ndiyo maana zipo nchi sasa zinalipwa fidia kutokana na vita vya dunia".
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad