Kimenuka Yanga Kakolanya Akimbia Kambini Usiku wa Manane

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mambo ni Moto Yanga Kakolanya Akimbia Kambini Usiku wa Manane
KIPA namba moja wa timu ya Yanga, Beno Kakolanya ameondoka kwenye kambi ya timu yake hiyo usiku wa manane wakiwa hotelini kwa madai kuwa hajatimiziwa makubaliano ya kimaslahi yaliyoko kwenye mkataba wake.



Hayo yamesemwa jana na Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera mara baada ya mchezo kati ya timu hiyo na Bishara United ya Mara ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 2-1 na kujikita kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.



Zahera amesema siku ya tukio hilo, timu ilikuwa imepumzika hotelini, lakini ilipofika saa saba usiku, Kakolanya aliamka na kwenda kukonga kwenye chumba ambacho alikuwa amelala mwalimu wake huyo kisha kumwambia yeye anaondoka kwa sababu Yanga hawajamtimizia makubaliano yao ikiwemo signing fee ambayo anadai alipewa nusu lakini nusu nyingine hajamaliziwa hadi leo.



Zahera anadai alimsihi abaki kwa sababu hata wachezaji wenzake wengi waliyosaini mwaka huu wakiwemo Makambo, Mrisho Ngassa bado hawajapewa pesa zao lakini wanaitumikia timu, Kakolanya aligoma na kuondoka mpaka leo hajarejea kambini na hata akipigwa simu na viongozi hapatikani.



Aidha, Kocha huyo amesema hawezi kusumbuka kumtafuta mchezaji kwani ni mechi nyingi amecheza bila mastaa lakini ameshinda na hajafungwa mpaka sasa. Pia ameongeza kuwa ni jambo la hatari kwa mchezaji kama Kakolanya ambaye anaichezea Yanga lakini wakala wake ni kiongozi ndani ya timu pinzani ya Simba.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad