Msekwa Awajibu Waliponda Baada ya Kuteuliwa na Rais Magufuli Kuwa Mkuu wa Chuo MUST

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Spika wa  Bunge Mstaafu, Pius Msekwa amesema uteuzi wake wa kuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) uliofanywa na Rais John Magufuli Desemba 6 ,2018 hakukosea na kwamba anatambua utendaji wake na uzoefu alionao kwa kuongoza baadhi ya vyuo vikuu nchini Tanzania kikiwapo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm).

Alisema hayo jana Jumamosi Desemba 15, 2018 alipokuwa akizungumza katika mahafali ya sita ya chuo hicho, ambapo alikuwa kivutio kutokana na staili yake ya kutumia vifungu vya biblia na kutoa mifano ya namna alivyokuwa akiliendesha Bunge.

"Kwanza kuna kila sababu ya kumshukuru Rais kwa kuniona mimi nafaa kuvaa kiatu hiki kwani kuna watu wengi serikalini lakini kaona mimi ndiye sahihi zaidi, nitaitumia fursa hii kuboresha elimu ya sayansi na teknolojia sambamba na kuongeza udahili kwa mwaka 2019/2020," alisema.

Msekwa alisema kupitia nafasi hiyo atahakikisha chuo hicho kinakuwa chachu ya kuzalisha wataalamu wa nyanja mbalimbali na kwamba amekuwa na bahati ya kuteuliwa kwa awamu ya tatu sasa kuongoza vyuo vikuu nchini.

Naye mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, Zakia Meghji alishauri uongozi wa chuo hicho kufanya tafiti katika nyanja mbalimba ili kuchochea maendeleo ya uchumi wa viwanda.

Alisema mafanikio ya chuo hicho yanatokana na jitihada za Serikali kutatua changamoto zinapojitokeza.

Makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Joseph Msambichaka alisema wana mikakati ya kuanzisha mfuko kwa ajili ya kusomesha wanafunzi wa  kike sambamba na kujenga maabara ya kisasa itakayochukua wanafunzi 2,000 kwa wakati mmoja.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad