1/14/2019

Huddah Awatolea Povu Zito Wasanii wa Kenya Kisa Play Kenyan Music

Huddah Awatolea Povu Zito Wasanii was Kesha Kisa Pray Kenya Music
Mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe amefunguka mtazamo wake wa kwanini? anapenda sana kusikiliza nyimbo za wasanii wa Nigeria kuliko Kenya.

Huddah kupitia Instagram Stories, amesema kuwa muziki wa Nigeria unahusisha maisha halisi ya kwenye jamii. Huku akiuponda muziki wa Kenya ambao amedai kuwa nyimbo nyingi ni za mapenzi, zina sifia ulevi na madawa ya kulevya .

“Unajua kwanini huwa huwa nasikilisa sana muziki wa Nigeria? unaniingia sana moyoni, kwa sababu nasikiliza kile kitu nataka kusikiliza, wenzetu wameamka sana. Ujumbe uliopo kwenye nyimbo zao sio tu mapenzi na madawa ya kulevya, bali wanazungumzia maisha halisia. Kiukweli wananivutia, na hivyo ndio vitu tunataka kusikia. Na sio kila siku kuimbia ngono, mapenzi na madawa ya kulevya,” ameandika Huddah .

Kwa upande mwingine Huddah amewapongeza wasanii kama Nyashinski, Sauti Sol, Octopizzo na Khaligraph Jones kwa kufanya muziki mzuri na kuitangaza Kenya kimataifa .


Kwa sasa nchini Kenya kuna kampeni ya PLAY KENYA MUSIC inayoshinikiza Radio&TV nchini humo kucheza muziki wa ndani kwa asilimia kubwa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger