Jerry Muro Aamuru Kuweka Ndani Diwani wa Chadema

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jerry Muro Aamuru Kuweka Ndani Diwani wa Chadema
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ameamuru kuwekwa ndani mmoja wa madiwani wa viti maalum wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa kosa la kuchukua mifuko ya saruji kinyume na utaratibu kisheria.

Akizungumza wakati akitangaza uamuzi wa kumuweka kiongozi huyo ndani, Jerry Muro amesema diwani huyo aliyefahamika kwa jina la Dinna Erick Mbise kuwa alikabadhiwa mifuko ya saruji 41, na moja ya wawekezaji wilyani humo ambapo hakuikabidhi kwa shule husika.

Muro amesema,"Diwani huyo wa CHADEMA amechukua mifuko iliyotakiwa kwenye kujenga shule na yeye hakupeleka wiki nzima, tukisema tunaambiwa tunaowaonea wao ni CHADEMA, lakini si kitu kizuri."

"Hii ni moja ya sehemu inayofanywa na wenzetu kutukwamisha, wanazunguka kuhamasisha watu wasituchangie huku ni kutuhujumu kabisa tukiwashughulikia mnatusema hatuna demokrasia. Tunajua mmepanga kutuhujumu lakini tutawashughulikia tu", ameongeza Jerry Muro.

Mara kwa mara Mkuu huyo wa Wilaya amekuwa akiingia kwenye migogoro na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutokana na sababu mbalimbali kutokana na kupishana mitazamo ya masuala mbalimbali nchini.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad