Kocha Azam Aipa Mbinu Simba ya Kupenya Kimataifa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kocha Azam Aipa Mbinu Simba ya Kupenya Kimataifa
KOCHA Mkuu wa timu ya Azam FC, Hans Pluijm ambaye amefanikiwa kukaa kwa muda mrefu kwenye Ligi ya bongo pamoja na kufanikiwa kushiriki michuano ya kimataifa amewapa mbinu kali Simba ili waweze kuwaua wapinzani wao mapema kwenye hatua ya makundi.

Pluijm ambaye alifanikiwa kuifikisha Yanga hatua ya makundi ya Shirikisho, amesema anaamini Simba wananafasi kubwa ya kupata matokeo iwapo wataamua kushirikiana.

Pluijm amesema ushindani kwenye hatua ya makundi ni mkubwa hasa ukizingatia kundi ambalo wamepangwa wana nafasi ya kupenya iwapo hesabu kubwa zitakuwa ni kushinda.

"Ushindani kwenye hatua ya makundi hasa wa Ligi ya Mabingwa sio sawa na huu wa kwenye Ligi Kuu Bara, nafasi pekee ambayo itawasaidia kuweza kupata matokeo ni kucheza wakiwa ni timu na siyo kumtegemea mchezaji mmoja.

"Kundi lao lina timu nzuri hawapaswi kubeza, timu zote zimejipanga na wajue kwamba kipindi cha kwanza kwa wapinzani huwa ni za ushindani hivyo wanapaswa kuwadhidibiti mapema na kupata matokeo ya haraka," alisema Pluijm.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad