1/14/2019

Trump atishia kuuangamiza uchumi wa Uturuki kuhusu Wakurdi Syria

Trump atishia kuuangamiza uchumi wa Uturuki kuhusu Wakurdi Syria
Rais wa Marekani Donald Trump ametishia 'kuiangamiza Uturuki kiuchumi' iwapo taifa hilo litawashambuliwa vikosi vya wakurdi nchini Syria baada ya wanajeshi wa Marekani kuondoka Syria.

Katika ujumbe wake alioutuma kwenye mtandaoi wa kijamii Twitter, Trump amesema hakutaka Wakurdi kwa upande wao nao pia waichokoza Uturuki.

Vikosi vya Marekani vimepambana kwa ushirikiano na wanamgambo wa Kikurdi kaskazini mwa Syria dhidi ya kundi la Islamic State (IS).

Uturuki hatahivyo inatazama wapiganaji hao wa vitengo vya YPG kama magaidi.Rais Recep Tayyip Erdogan amezungumza kwa hasira kuhusu Marekani kuliunga mkono kundi hilo, na kuapa kuliangamiza.

Kauli ya Trump Jumapili inafuata shutumza zaidi dhidi ya uamuzi wake wa ghafla kuondosha vikosi vya Marekani kutoka Syria.

Afisa mkuu kutoka familia ya kifalme Saudia, Prince Turki al-Faisal, ameiambia BBC kwamba itakuwa na 'athari mbaya' ambayo huenda Iran, rais wa Syria Bashar al Assad na Urusi zikafaida kutokana kwayo.

Waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo kwa sasa yuko katika mji mkuu wa Saudia Riyadh anapozuru Mashariki ya kati kuwahakikishia washirika wa Marekani katika eneo.

Trump amesema nini?

Rais ametetea uamuzi wake kuondoa vikosi, akieleza kuwa wapiganaji wowote waliosalia wa IS wanaweza kushambuliwa kutoka eneo ambalo halikutajwa, 'lililopo katika kambi za karibu'.

Hakueleza namna uchumi wa Uturuki utakavyoathirika iwapo taifa hilo litawashambulia wapiganaji wa YPG. Trump pia ametaja kuundwa kwa 'eneo salama la maili 20' ambalo mwandishi wa BBC Barbara Plett Usher anasema linadokezea aina ya suluhu ambayo Pompeo anajaribu kuijadili.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger