Alichokisema Katibu Mkuu CHADEMA Baada ya Maalim Seif Kuhamia ACT- Wazalendo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt Vincent Mashinji amempongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF kwa hatua yake ya kujiunga na Chama cha ACT- Wazalendo na kusema uamuzi wake ni sahihi.

"Nimpongeze kwa uamuzi wake wa kuendelea na shughuli za kisiasa na kupigania mabadiliko kwenye taifa letu, watu wengi walitegemea yeye kupumzika lakini amejipima na ameona anahitaji kuendelea kufanya kazi ni hatua kubwa kwetu sisi wapinzani." Amesema  Dkt Vincent Mashinji

Mapema leo Machi 18, 2019 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam, ilitangaza kutambua uhalali wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba.

Kufuatia maamuzi hayo ya Mahakama,  majira ya saa nane leo Machi 18, 2019  Maalim Seif alitangaza uamuzi wa kuhamia Chama Cha ACT- Wazalendo

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad