Amber Rutty Afunguka Sababu ya Kumrudisha Shule

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Amber Rutty Afunguka Sababu ya Kumrudisha Shule
Video Vixen, Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Ruth’ amesema ameamua kurudi shule baada ya kugundua elimu ni kila kitu anachokihitaji kwa sasa katika maisha yake.

Akizungumza na www.eatv.tv, Amber Ruth, amesema kwamba kutokana na matatizo mengi aliyopitia ameamua kurudi shule kwani ndiko sehemu ambayo anaona anapata amani ya moyo ikiwa ni pamoja na kupoteza Stress.

Mwanadada huyo asiyekaukiwa matukio amesema kwamba baada ya kuacha shule 2009 akiwa kidato cha pili, kwa sasa ameanza kidato cha tatu katika shule ya kulipia yeye na mume wake.

Sababu nyingine iliyomfanya Amber Ruth kurudi shule ni kutaka kufahamu vizuri lugha ya kingereza kwa kuwa inamsumbua sana hasa anapokutana na watu wasiojua lugha ya kiswahili.

Akizungumzia kuhusu wanafunzi wengine wanavyomchukulia, Amber anasema japo wapo watu wengine wanaombeza kwa kitendo kilichowahi kumtokea lakini ni tofauti na kushinda mtaani ambapo ndipo kunampelekea hadi kulewa ili kupoteza mawazo.

Kuhusu kuacha kushiriki matamasha ya usiku, amesema atazidi kushiriki kwa kuwa ndipo anakopatia fedha za matumizi mbalimbali na shule anayosoma haimzuii kufanya hayo.

Amber Ruth anakabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile analodaiwa kulitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad