4/17/2019

Alichokubali Kufanya Chris Brown Katika Kesi ya Ubakaji Inayomkabili

Alichokubali Kufanya Chris Brown Katika Kesi ya Ubakaji Inayomkabili
Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeripoti kuwa mwimbaji Chris Brown amemruhusu mwanamke anayefahamika kwa jina la Jane Doe kufanya ukaguzi kwenye nyumba yake mjini Los Angeles baada ya mwanamke huyo kumfungulia shtaka la ubakaji miezi kadhaa iliyopita.

Inaelezwa kwa mujibu wa nyaraka za Mahakama zitamruhusu Jane Doe kufanya ukaguzi katika nyumba hiyo akisindikizwa na wakili wawili pamoja na mpiga picha kwa ajili ya kufanya uchunguzi ndani ya vyumba vyote na huenda akakumbuka mazingira aliyekuwepo kipindi anafanyiwa tukio hilo. Jane Doe ataruhusiwa kurekodi tukio zima bila video hizo kuwa na sauti.

Inaelezwa Breezy ana haki ya kupinga chochote ikiwemo na kupewa nafasi ya kurekodi kila tukio litakaloendelea na pia kuondoa vitu ambavyo ni vya msingi ndani ya vyumba hivyo na inabidi apange tarehe za kuwaruhusu kufanya ukaguzi huo huku mahakama ikiwa imetoa siku 120 ili ukaguzi huo uwe umekamilika.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger