4/15/2019

Rose Muhando Yupo Fiti Aruhusiwa Kutoka Hospital Kenya

MWIMBAJI  maarufu wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando, hatimaye ameagwa katika hospitali aliyokuwa amelazwa nchini Kenya baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Rose ambaye aliibua hisia kali miongoni mwa mashabiki wake nchini Kenya na Tanzania miezi minne iliyopita alipoonekana jijini Nairobi akiwa na majeraha makubwa na akiombewa na mhubiri wa Neno Evangelism jijini Nairobi, James Nganga, ameonekana akiwa na waimbaji wenzake wa nyimbo za dini, Betty Bayo, Solomon Mkubwa na wengine.

Katika picha hizo, majeraha aliyokuwa nayo hayaonekani tena na anaonekana ni mchangamfu kabisa ikiashiria hali yake ya kiafya ikiwa imeimarika huku uso wake uking’aa na mwenyewe akitabasamu kutokana na matendo makuu ya Mungu aliyemponya.

Katika video iliyochapishwa na Solomon Mkubwa, anaonekana akiimba na kumshukuru Mungu kwa kumponya.

Solomon ame-post picha akiwa na Rose na waimbaji wengine na kuandika: “Mungu mukubwa Rose muhando amekua vizuri. Malkia Rose yuko poa sasa.”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger