Wezi Walivyonaswa na Camera Wakiiba Ofisini Dar Bila Kujua Wanarekodiwa, Boss kaongea (Video)


Teknolojia ya camera za video zinazorekodi saa 24 ndani ya Ofisi imemuwezesha Mfanyabiashara wa Dar es salaam Wesley Lema kuwatambua kwa sura Wezi walioingia Ofisini kwake na kuona jinsi walivyomuibia computer mbili aina ya laptop.

Tukio lilitokea Jumamosi lakini alikuja kushtuka Jumatatu baada ya Vijana wake kuingia kazini na kumwambia hawazioni laptop za kufanyia kazi ndipo walipokwenda kwenye kumbukumbu za camera za usalama na kupata jibu kwamba wezi ndio waliingia kwenye Ofisi hiyo siku ya Jumamosi.

Baada ya kugundua Wizi huo Lema alisambaza msg kwenye Whatsapp group mbalimbali ili yeyote anaewatambua Wezi hawa ampe taarifa au aripoti Polisi

“Wapendwa Jumamosi vibaka waliingia Ofisini kwetu na kuiba Laptop mbili, kama unawatambua tafadhali piga simu no 0715685099 au toa taarifa kituo chochote cha Polisi CD/RB/2365/2019” 
VIDEO:


HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Wezi Walivyonaswa na Camera Wakiiba Ofisini Dar Bila Kujua Wanarekodiwa, Boss kaongea (Video) Wezi Walivyonaswa na Camera Wakiiba Ofisini Dar Bila Kujua Wanarekodiwa, Boss kaongea (Video) Reviewed by Udaku Special on April 14, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.