Rais Mnangagwa Amfukuza Kazi Waziri was Nishati Kisa Mgao wa Umeme

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amemfukuza kazi waziri wa nishati, Joram Gumbo kwa sababu ya tatizo la kukatika umeme mara kwa mara tangu mwaka 2016.

Nafasi ya waziri huyo amepewa naibu waziri wa usafirishaji na miundo mbinu Forune Chasi.

Gumbo sasa amepewa wadhifa wa kuwa waziri katika ofisi ya rais ,kufuatilia utendaji na utekelezaji wa idara za serikali.

Kiwanda hicho kinachomilikiwa na serikali amesema siku ya jumatatu kuwa umeme ambao umekuwa ukikatika kwa saa tano au nane kutokana na upungufu wa maji katika mtambo mkubwa wa uzalishaji umeme.


Zimbabwe imekuwa ikipata tatizo la ukataji umeme tangu mwaka 2016
Siku ya jumatatu , kampuni ya uzalishaji umeme inayomilikiwa na serikali ilitangaza kuwa umeme utakatika kwa saa tano mpaka nane.

Vilevile machimbo ya migodi yatahathirika na kukatika huko kwa umeme.

Mamlaka inalaumu kuzimika au kukatika kwa umeme huo kutokana na mtambo wa uzalishaji umeme kuzalisha umeme kwa kiwango kidogo kutokana na ukame ambao umesababisha maji kupatikana kwa kiwango kidogo.

Baadhi ya nchi jirani wamedai kuwa umeme kwao umewahi kukatika kwa muda mrefu zaidi hadi saa 10.

Aidha serikali ya Zimbabwe imepanga kuagiza nishati kutoka nchi jirani ya Msumbiji na Afrika kusini.

Kabla ya mwaka 2016, tatizo hilo la umeme limezua gumzo katika mitandao ya kijamii tangu wakati huo mpaka sasa .
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad