5/19/2019

Shuhudia Jinsi Mwanamke Alivyochepuka Kiboya na Kinashwa

Mke alimuaga mumewe anaenda kumsalimia mama yake mgonjwa kijijini. Akaondoka Ijumaa na kurudi Jumatatu na matunda kibao na vyakula vingine toka kijijini akisema ni mama kanipa kwa ajili yako mume wangu na watoto, mume akamuuliza kwa upole mama anaendeleaje?

Mke akajibu amempeleka hospitali ila anaendelea vema, mke aliongezea kwamba mama yake amemsisitiza amtembelee tena baada ya siku chache akae naye wiki, nina hofu na afya ya mama mke aliongea kwa uchungu huku machozi yanamtoka.

Mume akamjibu kwa huruma atapona mpenzi usijali. Mume akamwambia kwa hekima ingiza vitu alivyoleta jikoni.

Mke ile anaingia jikoni anamkuta mama yake mzazi akiandaa chakula jikoni. Kumbe mama ake alikuja kumtembelea tangu Ijumaa yeye alivyoondoka. Mke akabaki ameduwaa mlangoni mwa jiko asijue apeleke vitu jikoni au arudi sebuleni kwa mume wake.
Je ingekuwa wewe ungefanyaje.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger