Peter wa Liquid Kuambatana na Wabunge 40 Kuishangilia Taifa Stars Misri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema wabunge 48 watakwenda kuishangilia timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazofanyika nchini Misri wakiambatana na Peter Mollel maarufu kama Pierre Konki Liquid.

Pierre  ni mmoja wa wachekeshaji wakubwa nchini.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Jumanne Juni 18, 2019 Ndugai amesema wataambatana na mchekeshaji huyo katika fainali hizo huku akiwataka wabunge zaidi kujiandikisha ili kwenda Misri.



“Hizi fainali ni muhimu na ninawashauri wabunge ambao hawajajiandikisha wafanye hivyo ili tukaishangilie timu yetu na kutembelea maeneo mbalimbali huko Misri,” amesema Ndugai.

Wiki iliyopita Ndugai alisema wabunge wanaotaka kukaa siku nne Misri wanatakiwa kulipia Dola 720 za Marekani (sawa na Sh1.7 milioni), wanaotaka kukaa siku 10 watapaswa kulipia Dola 1,490 (sawa na Sh3.5 milioni).

Katika fainali hizo zitakazoanza Juni 21 hadi Julai 19, 2019, Taifa Stars imepangwa kundi moja na Algeria, Senegal na Kenya.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad