Ni VITA Kati ya WanaCCM Asilia na Wahamiaji?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Na Thadei Ole Mushi.

Wakati Mwita Waitara ailipohamia CCM na Kuukwaa uwaziri akiwaacha vijana wengi pale Lumumba na maeneo mengine wa CCM wanaokesha usiku na mchana kuimba Litania za Masifu na Mapambio niliandika naomba kunukuu

“Karibu Mwita Waitara CCM, Karibu kwenye chama kinachoongoza nchi. Wakati tukilala nje 2015 tukitafuta kura za rais wetu John Pombe Magufuli wewe ulikuwa ukilala nje kuzipunguza..

Hii ndio aina mpya ya siasa zetu, zimebadilika na lazma tukubali kubadilika nazo. Ni siasa nazoweza kuzifananisha na mtu aliyewanyima watoto wake wa kuwazaa chakula na kuamua kuwalea watoto wa jirani.

Wenzetu wamelisoma gape kuwa upande wetu tumekusanyika wale wenye uwezo mdogo kiuongozi. Ni sawa na mtoto anayesoma seminari kuhamia Shule ya Kata lazma awaongoze.

Mpaka kufikia 2019-2020 ngome ya CCM asilia itakuwa imeshatekwa yote na tutakuwa mateka haswa.

Hongereni wapinzani kwa kuivisha viongozi wa taifa hili. Nimeamini ninyi ni tanuru la uongozi nchini…. sisi CCM lazma tujitathimini sana. Tufanye pia na utafiti kuangalia wanachama wa ANC na ZPF kama aina hii ya siasa inaweza kufanyika. Yaani wanachama wao wapoje…

#Unapata wapi Ujasiri wa kuwaita Nyumbu wakati wana uwezo kuliko wewe?
Karibuni sana CCM”

Mwisho wa kunukuu, usimkumbuke Patrobas, wala kina Shonza, usimkumbuke Kafulila wala machali, usimkumbuke Msando aliyepewa kazi ya kuhakiki mali za CCM wala Mwita waitara twende na Mtatiro aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa Sera za CCM na Rais wetu.

Huyu naye anatokea Timu iliyopunguza kura za JPM hadi tukaamua kupiga Pushup ili zitoshe. Hasa ndio waliohakisha kwa Mara ya kwanza CCM inaingia madarakani kwa ushindi cini ya asilimia 60.

Ni Julias Mtatiro aliyeitwa nyumbu na vijana wa Lumumba anaukwaa u DC pale mkoani Ruvuma…… Narudia msiwaite wenzenu nyumbu hata kidogo…… Mtag mwanaccm yeyote muimba pambio na litania za masifu. Watapishana na Mtatiro kwa adabu sasa hivi maana anaweza msweka ndani 24 hours.

Kila wazee wa vetting wakichakura kwenye hill jalala la Lumumba wanakutana na wasiokidhi vigezo. Sijui kwa nn CCM inapendwa na wasiokuwa na uwezo huku upinzani ukiwa na vijana very Smart. Hapa ndipo huwa sielewi kuwa CCM inapenda wasiokuwa na uwezo au wasiokuwa na uwezo ndio huipenda CCM.

OLE Mushi
0712702602
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad