8/13/2019

Nick Minaj Apewa Siku 80 Kukamilisha Mipango ya Ndoa

Nicki Minaj apewa siku 80 kukamilisha mipango ya ndoa
Baada ya mtandao wa TMZ kuripoti kuhusu rapper Nicki Minaj pamoja na mpenzi wake Kenneth Petty kufanikiwa kupata leseni yao ya ndoa siku kadhaa zilizopita sasa ripoti mpya imewekwa wazi kuwa wawili hao wamepewa siku 80 za kukamilisha mipango yao ya ndoa.

Kupitia Queen Radio ambayo inamilikiwa na Nicki Minaj aliweka wazi kuwa yeye pamoja na mpenzi wake waliwahi kupata leseni ya ndoa lakini hawakukamilisha ndoa hiyo kutokana na ratiba walizokuwa nazo na hivyo leseni hiyo iliisha muda, sasa kupitia leseni hii ya pili inawataka wafunge ndoa ndani ya siku 80.

Nicki Minaj na Kenneth  waliingia kwenye mahusiano mwaka jana 2018 na kuelezwa kuwa walikutana kwa mara ya kwanza Nicki akiwa na umri wa miaka 17 hivyo hii itakua ndoa ya kwanza kwa Nicki Minaj. Pia Nicki ameeleza kuwa harusi yao itakuwa ndogo na mbeleni watapanga sherehe kubwa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger