Wafanyabiashara 300 kutoka Uganda kutua Tanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania mapema mwanzoni mwa mwezi Septemba, ambapo atakutana na kufanya majadiliano ya fursa za uwekezaji miongoni mwa nchi mbili na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Taarifa hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Balozi wa Uganda nchini, Richard Kabonero ambaye ameeleza kuwa Rais Museveni anatarajiwa kuwasili nchini Septemba 6, 2019.

Aidha, ameeleza kuwa kabla ya ziara hiyo kutakuwepo na ujio wa wafanyabiashara zaidi ya 300 kutoka nchini humo kuhudhuria jukwaa la biashara baina ya wawekezaji wa Tanzania na Uganda.
”Wiki ijayo kutakuwa na mkutano mkubwa hapa, Rais wetu atakutana na Rais mwenzake Rais Magufuli, kuhusu wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda, tuko na Waganda kama 300 watakuja” amesema Balozi Kabonero.

Balozi Kabonero amesisitiza kuwa, majadiliano hayo ndiyo mwanzo wa mkakati wa ushirikiano wa kuboresha mahusiano ya kimaendeleo, katika sekta mbalimbali ikiwemo usafiri wa anga.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad