9/15/2019

Fahamu Sababu za Mwenyekiti Simba KujiuzuluLeo Septemba 14, 2019 uongozi wa klabu ya Simba umetoa taarifa kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedi Mkwabi amejiuzulu nafasi yake.Taarifa hiyo imeeleza kuwa Swedi ameiandikia Barua Bodi ya Wakurugenzi kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mohammed Dewji, ambapo ameeleza sababu kuu ya kijiuzulu nafasi hiyo ni kuhitaji muda zaidi kusimamia shughuli zake binafsi.

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba pamoja na Sekretarieti ya Simba imemtakia kila la heri katika shughuli zake.

Lakini pia imeeleza kuwa ina imani ataendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za klabu kama ilivyokuwa awali kabla kupata nafasi hiyo.

Aidha imebainisha kuwa utaratibu wa kumpata Mwenyekiti mpya utatangazwa.
TAZAMA WIMBO MPYA WA ROSA REE

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger