9/19/2019

Makahaba 4 Jela Miezi 6 na Viboko 3 vya Nguvu...


Wanawake wanne ambao wanajihusisha na Ukaaba na Mwanaume Mmoja ambae anadaiwa kuwa Mteja wao wamehukumiwa kifungo cha miezi sita Jela na mahakama ya mwanzo Makole, Mkoani Dodoma pamoja na kuchapwa viboko vitatu kila mmoja wakati wanaingia jela.

Hukumu hiyo inatolewa baada ya jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kuendelea na msako wa kuwakamata Wanawake wanaodaiwa kuwa Makahaba katika maeneo mbalimbali Mkoani hapo ambao wanafanya kazi ya kuuza mili yao kama sehemu ya kujiingizia kipato.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muruto alisema Msako wa wakina dada ambao wanauza mili yao unaendelea na kuwataka wanaofanya biashara hiyo kuacha mara moja.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

1 comment:

  1. Hapana si haki kufanya msako wa kukamata akina dada pekee. Bali msako wa haki ni ule wa kusaka wateja. Sheria ibadilike na zoezi la kusaka makamba liboreshwe na haki izingatiwe. Mbona rushwa imewezekana? Mitego ya rushwa naamini inaweza kutumika katika kusaka makahaba wake kwa waume bila kupendelea

    ReplyDelete

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger