Menina Asimulia Video Yake Chafu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MWIGIZAJI na msanii wa Bongo Fleva nchini, Menina Abdulkarim ‘Meninah’ hatimaye jana alijisalimisha kwenye Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa ajili ya kutoa maelezo ya video na picha zake za utupu zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii. Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu Basata imuite msanii huyo ofisini kwa ajili ya kutoa maelezo ya video na picha hizo chafu zilizozagaa na kuzua mijadala mikubwa.



Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza ameliambia gazeti hili kuwa kupitia utaratibu wao wa kutoa elimu kwa wasanii na umma wamekuwa wakiwaelekeza wasanii kote nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili mema kwa jamii na kufuata taratibu za kujisajili.


Alisema kwa bahati mbaya baadhi ya wasanii wamekuwa hawazingatii maelekezo hayo na hivyo kujikuta wanavunja sheria za nchi. Mngereza alisema kupitia mahojiano kati ya Meninah na Basata, baraza wamesikiliza maelezo ya msanii huyo juu ya nini kilichojitokeza katika sakata la kusambaa kwa video zake za utupu kupitia mitandao ya kijamii.



“Basata ilisikiliza maelezo yake ambayo watayafanyia kazi, baada ya hapo baraza litakaa kujadili suala hilo, hatukuanza kwa Meninah wasanii wengi tuliwaita kuzungumza nao kwa kosa kama hilo lake,” alisema Mngereza.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad