Bobi Wine akamatwa na polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Polisi wamefyatua risasi na mabomu ya machozi kuwasambaratisha watu wanaomuunga mkono Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, mbunge wa eneo la Kyandondo Mashariki, aliyekamatwa kabla ya kufanyika kwa mkutano wake wa kwanza wa kutafuta kuungwa mkono katika wilaya ya Wakiso.

Bobi Wine alikamatwa pamoja na wabunge wengine Asuman Basalirwa, Latif Ssebagala,Waiswa Mufumbira na mwenyekiti wa baraza la Kasangati na kwa sasa wanashikiliwa katika kituo cha polisi cha Kasangati.

Gazeti la The Observer limemnukuu Basalirwa akisema walikuwa wakiendesha gari la Kyagulanyi kabla ya polisi kuwazuia katika eneo la Kasangati na kuwapeleka katika kituo cha polisi. Kyagulanyi alikuwa akitarajiwa kuzindua mikutano ya mashauriano kuhusu malengo ya urais kwa uchaguzi mkuu ujao.

Polisi wamedai kuwa ilibidi kuuzuia mkutano huo kwa sababu ulipangwa kufanyika kwenye eneo la wazi, wakati mikutano ya namna hiyo hufanyika ndani ili kutoingilia shughuli za watu wengine.

Pia polisi wamedai kuwa hakukuwa na vyoo vya kutosha kwa ajili ya wageni waliokuwa wakitarajiwa.

Mbunge huyo aliiandikia tume ya uchaguzi kabla ya krisimasi akieleza nia yake ya kufanya mkutano kitaifa kuhusu nia ya kuwania urais. Ingawa alitoa taarifa kwa tume hiyo, ambayo ilimruhusu, imesema hakutimiza vigezo vingine kama vinavyoelezwa kwenye sheria.

Bobi Wine ameeleza nia yake ya kuwanida urais dhidi ya rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.

Gazeti la Daily Monitor lilimnukuu Bobi Wine siku ya Ijumaa akisema kuwa kuwa sheria ya uchaguzi inampa fursa ya kuzungumza na watu kuhusu kama watamuunga mkono katika mipango yake ya kuwa mgombea kwenye uchaguzi ujao wa urais mwaka 2021.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad