Mfamasia Kizimbani kwa Kuiba Dawa za Kufubaza Ukimwi (ARV)

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mfamasia wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora, Francis Mlesa (33), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa wilaya hiyo kwa tuhuma za wizi wa dawa za wagonjwa Mwendesha Mashtaka, Joseph Mwambwalu, alidai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na shtaka moja la wizi.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Edda Kahindi Mwambwalu, alidai Desemba 24, mwaka jana majira ya usiku, katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, mtuhumiwa akiwa mwajiriwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, anatuhumiwa kuiba chupa 30 za vidonge vya dawa ya kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARV) zenye thamani ya Sh. 2,116,000.

Mwambwalu, alidai kuwa huku mshtakiwa huyo akitambua kwamba yeye ni mtumishi wa umma, aliamua kutenda kosa hilo kinyume cha kifungu 270 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

Hata hivyo, baada ya mshtakiwa huyo kusomewa shtaka lake, alikana na hakimu kuiahirisha kesi hiyo hadi Januari 31, mwaka huu, na mshtakiwa yuko nje kwa dhamana ya Sh. 300,000 kwa maandishi.


----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad