3/31/2020

Wakati Nchi Nyingine Zikisita Kutekeleza Adhabu ya Kunyongwa, Botswana Yaua Watu Wanne KisheriaBotswana, ni moja kati ya nchi za kidemokrasia zinazoendeleza adhabu ya kifo. Machi 28, 2020, Moabi Seabelo Mabiletsa (33) na Matshidiso Tshid Boikanyo (39) walinyongwa hadi kufa katika mji mkuu wa Botswana, Gaborone

Wawili hao walimuua dereva wa taksi miaka sita iliyopita. Kabla ya hawa kuna mwingine alinyongwa mwezi Februari na mwingine mwezi Desemba mwaka jana. Hii ndio nchi pekee kusini mwa Afrika inayotekeleza adhabu ya kunyongwa

Hii inafanya jumla ya watu wanne kuwa wamenyongwa tangu rais Mokgweetsi Masisi achaguliwe kuingia madarakani Aprili 1, 2018. Adhabu ya kifo ipo kisheria tangu walipopata uhuru wao toka kwa Uingereza mwaka 1966

Kwa mujibu wa Amnesty International, nchi 195 duniani zimefuta adhabu ya kifo au wameacha kuzitekeleza kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger