Utafiti Mpya Chanjo ya COVID-19 Waonesha Matumaini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Utafiti Mpya Chanjo ya COVID-19 Waonesha Matumaini

Utafiti wa jarida la kitabibu la The Lancet umeonesha chanjo ya COVID-19 ya China imeleta matumaini baada ya kujaribiwa kwa watu wazima 108 wenye umri wa miaka 18 hadi 60 katika jimbo la Wuhan.

Matokeo ya awali kutokana na jaribio la watafiti wa  nchini China yameonesha chanjo hiyo ni salama, himilivu na yenye uwezo wa kuzalisha kinga dhidi ya  SARS-COV-2 ambavyo ni visababishi vya COVID-19 kwa binadamu.

Utafiti huo umeonesha matumaini katika siku 28 za kwanza ambapo matokeo ya mwisho yanatarajia kutolewa ndani ya miezi sita, huku Profesa wa kitengo cha magonjwa ya kuambukiza na afya ya jamii katika Chuo Kikuu cha California, Robert Schooley akisema chanjo hiyo ni himilivu.

"Chanjo imeonesha kuwa ni himilivu kutokana na dozi tatu zilizojaribiwa na watu waliojaribiwa wameonekana kutengeneza kinga dhidi ya virusi vya Corona", amesema Prof. Schooley.

Prof. Schooley amesema kuwa utafiti zaidi unatakiwa kufanyika ili kubaini endapo nguvu ya kinga ya mwili itakuwepo na kinga ya T-cells inayopatikana mwilini itaendelea kupungua baada ya siku 28 huku akitaja umuhimu wa dunia kuungana katika utafiti wa maendeleo ya chanjo ya COVID-19 kwa pamoja
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad