5/27/2020

Rais Donald Trump wa Marekani Akosolewa na Mtandao wa Twitter Baada Ya Kutoa Ujumbe wa Upotoshaji

Rais Donald Trump wa Marekani Akosolewa na Mtandao wa Twitter Baada Ya Kutoa Ujumbe wa Upotoshaji

Mtandao wa kijamii Twitter umemkosoa Rais Donald Trump wa Marekani kwa kuchapisha katika mtandao huo wa kijamii taarifa za kupotosha kuhusu uchaguzi mkuu ujao wa nchi hiyo.

Twitter imesema ujumbe wa Trump kwamba kufanyika uchaguzi wa Novemba mwaka huu kwa njia ya kutuma baruapepe kutasababisha uchakachuaji wa matokeo; hauna ukweli wowote.

Trump anadai kuwa hizo ni njama za chama cha Democrats za kuiba kura katika uchaguzi huo.

Mwanasiasa huyo wa Repulican ameutishia na kuukosoa mtandao huo wa kijamii kwa kuuainisha ujumbe wake huo kuwa wa upotoshaji, na kuandika: Twitter inabinya kabisa uhuru wa kujieleza, na mimi kama Rais, sitokubali hilo lifanyike.

Trump amekuwa akiutumia mtandao huo wa kijamii kama jukwaa lake kuu la kutoa taarifa rasmi na zisizo rasmi, na hata kuwakebehi na kuwakejeli wapinzani na wakosoaji wake.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

2 comments:

 1. Je?, alipata idhini toka kwa Wazee wa twita kina Godilesi na Jitto.? vinginevyo hana Uhalali huo.
  Jitto/Godilesi, mlimruhusu?

  ReplyDelete
 2. Je?, alipata idhini toka kwa Wazee wa twita kina Godilesi na Jitto.? vinginevyo hana Uhalali huo.
  Jitto/Godilesi, mlimruhusu?

  Stimulasi pekeji na Rockdawni..!

  ReplyDelete

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger