5/25/2020

Wanawake, Msing'ang'anie Wanaume Ambao Hawawataki

Zaidi ya watu wa 5 wameshakueleza kwamba jamaa hana time na wewe na ameshachumbia mtu mwingine hukuamini. Mungu sio Mwigulu Nchemba, siku 1 akiwa kwenye mishemishe za kuchepuka simu yake ikajipiga ukamsikia anaongea na msichana mwingine na baada ya muda ukawasikia wanapiga kwinchi kwinchi Live wakati alikuaga muda huo yuko kwenye kikao cha harusi. Mungu akaamua kukuonyesha kitu live.

Ulipomuuliza akaruka futi elfu 6 kwamba unamsingizia una kila ushahidi kwamba huyo jamaa ni kimeo ila kwa sababu akili yako ina ujibwa ulezi uliochanganywa na alizeti ukamsamehe, sasa leo amekuoa na tabia zilezile walizokuonya rafiki zako zimeendelea, unashinda unalia na kuimba Pambio la bwana tenda miujiza usiaache mpaka mwaka huu upite.

Alishatenda muujiza kukuonyesha ushahidi hukutaka kumsikia, ukapenda zaidi matarumbeta ya harusi bila kujali ndoa itakuwaje. Pole hakuna muujiza hapo, jipigie matarumbeta kwa kujitendea muujiza. Kamwe usidharau Mungu akikuonyesha (clear Signs) kwamba mtu uliyenaye ni shida. Using'ang'anie kuwa mjumbe wa bunge la katiba kama unahisi posho haitoshi achia ngazi.

Heri ukose harusi leo ujiandae kwa ndoa bora ya keshokutwa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger