Hatimaye Kinana amuomba radhi Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi, Bw.Abdulrahaman Kinana amemuomba radhi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kwa matukio mbalimbali aliyoyafanya baada ya kuondoka katika uongozi wake. 

Pamoja na hayo Kinana amewaomba radhi pia Watanzania na Wanachama wa CCM kwa vitendo alivyovifanya. 

Kinana akiwa na baadhi ya viongozi wakongwe wa chama hicho walipewa adhabu  baada ya mazungumzo yao ya simu kunaswa wakimteta Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii hali iliyosababisha uongozi wa CCM kuwaita na kuwahoji viongozi hao. 

Awali akizungumzia adhabu aliyopewa na chama Kinana amekiri kutokea kwa jambo hilo na kudai kuwa kama binadamu alighafilika na kudai kuwa akiwa ni mkongwe katika chama hicho adhabu ni utaratibu uliopo katika chama chochote kwa kiongozi au mwanachama anapokosea. 

Wakati huo huo Komrade Kinana ametembea ofisi za CCM mkoa wa Arusha na kuzungumza na mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Arusha Zelothe stephen zelothe. 

Tangu sakata hilo litokee Katibu mkuu huyo mstaafu wa CCM hakuwahi kusikika katika vyombo vya habari wala mitandao ya kijamii kuzungumzia sakata hilo. 

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad