Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Katavi: Watu 15 wakamatwa kwa kumuozesha binti wa darasa la 5

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Jeshi la Polisi limewakamata Watuhumiwa 15 wakiwemo Wazazi 2 kwa kumuozesha Mwananfunzi wa darasa la 5 kwa mahari ya ng'ombe 12

Kamanda wa Polisi wa Mkoani humo, Benjamin Kuzaga amesema wamefanikisha kuisambaratisha ndoa hiyo ya kimila na wanaendelea na juhudi za kumtafuta muoaji ambaye alitoroka

Ndoa za Utotoni, chini ya miaka 18 (Wavulana na Wasichana) ni marufuku Tanzania kutokana na kushinda kwa kesi iliyofunguliwa mwaka 2016 na Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia ya Msichana Initiative, Rebecca Gyumi. Awali umri wa kufunga ndoa ulitofautiana kwa Wavulana na Wasichana

Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, Kifungu cha 148 (1&2) kinasema Mtu yeyote anayefunga ndoa huku akijua au akiwa na sababu ya kujua kuwa mwenza wake yupo chini ya umri wa ndoa atahukumiwa kifungo cha miaka 3

Pia, mtu yeyote anayakeshiriki katika ndoa hiyo atakuwa na kosa na atahukumiwa kifungo kisichozidi miaka miwili

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments