Marekani: Jengo la mahakama lachomwa moto wakati wa maandamano mjini California

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Waandamanaji mjini California wamechoma moto jengo la mahakama, wameharibu kituo cha polisi pamoja na kuwashambulia maafisa kadhaa wa polisi baada ya maandamano yaliyokuwa ya amani kugeuka na kuwa ya fujo hapo jana Jumamosi. 


Polisi ya Oakland imesema kupitia mtandao wakeTwitter kwamba waandamanaji hao walivunja madirisha, walichorachora kwa kupulizia rangi kwenye kuta na walirusha fataki na hata kuwaelekezea mionzi maafisa wa polisi. 


Polisi wamewataka waandaaji wa maandamano hayo kuhimiza amani.Maandamano hayo yalianza jana Jumamosi jioni ambapo baadae usiku waandamanji walikabiliana na vikosi vya usalama vilivyopelekwa mjini humo kuweka ulinzi kwenye jengo la mahakama. 

Rais Donald Trump amepeleka vikosi hivyo vya usalama kukabiliana na maandamano yanayofanyika kila usiku tangu kilipotokea kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd mjini Minneapolis mnamo mwezi Mei, 25. 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad