Mchungaji Akamatwa Akibanjuka na Mke wa Muumini, Aponea Kifo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwenye nyumba alifika nyumbani mapema na kumpata mchungaji wake akimla uroda mkewe kwenye kitanda chake

Mchungaji alitimka mbio akiwa nusu uchu huku akiacha pikipiki yake na baadhi ya nguo zake

Wenyeji walisisitiza kuwa lazima mchungaji huyo aombe msamaha kwa mume huyu pamoja na kumpa ngombe na mbuzi

Mchungaji mmoja wa Kakamega ameponea kifo baada ya muumini wake kumkamata ana kwa ana akimlambisha asali mkewe nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa mdakuzi wetu, mume huyo alirudi kutoka kazini mapema kinyume na ilivyokuwa desturi yake, kilichomshangaza ni pale alipompata mchungaji wake akiwa na mkewe kitandani mwake.

Kulingana na ripoti ya K24, mchungaji huyo wa kanisa la Solid Rock of Jesus Christ alilazimika kuchana mbuga kuepuka hasira ya muumini wake, akilazimika kuiacha pikipiki yake pamoja na baadhi ya nguo alizovua wakati wa maandalizi ya mzinga.

Chifu wa eneo hilo Alex Mutende alithibitisha kisa hicho huku akisema kuwa maafisa wa polisi walianza msako kumkamata mchungaji huyo na uchunguzi kuendelea.

DCI Intercepts Suspicious Somalis Aboard Police Vehicle - Kenyans ...

Mutende alieleza kuwa alichukua nguo za mchungaji huyo zilizosalia alipotoroka mbio pamoja na pikipiki yake.

Baadhi ya wenyeji waliofika katika eneo la kisa kwa hasira walimtaka mchungaji huyo kujitokeza na kuomba msamaha kwa mume huyu pamoja na kumpa ngombe na mbuzi kama njia ya kunyenyekea.

Jamaa huyo ambaye alijawa hasira alieleza kuwa hayuko tayari kumsamehe mchungaji huyo kwa madhara aliyoifanyia familia yake.

Wawili hao walikuwa wamejaliwa watoto watatu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad