7/14/2020

Nandy Amjibu Msanii Gigy Money "Ukitaka Vita na Mpare, Sogelea Huo Ungo "


Msanii Gigy Money pamoja na msanii mwenzie Nandy wameingia kwenye bifu zito, kitendo ambacho kimefanya wavunje uvumilivu wao na kuamua kutoleana 'Povu' LAIVU LAIVU.

Baada ya sintofahamu hiyo, Gigy money amefunguka Sababu kubwa iliyopelekea kuwepo na tofauti kati yake na Nandy .

Kama utakumbuka aliamua kwenda Live kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuzungumza mengi kuhusu Nandy na Maoni ya mashabiki ya yeye kujifananisha na Hit maker wa Acha Lizame .
.
Gigy money ameweka wazi kuwa Nandy Aliamua kumzunguka katika deal lake la Biashara ambapo Yeye ndiye aliyemtambulisha Nandy kwa Mfanya Biashara huyo kutokea Nigeria. Gigy ametoa ya moyoni pia na kusema kuwa Nandy ni mnafki na hampendi kabisaaaaa .
.
Akiendelea zaidi, Gigy amesema kuwa aliamua kuikataa show ya Diamond na kwenda kumsapoti Nandy katika Tamasha lake licha kutopewa Kiasi cha Pesa alichostahili lakini msanii huyo hana shukrani na ameendelea kumfanyia 'Unafiki'.

Baada ya matusi kadhaa ambayo sio sahihi kuyaandika hapa ambayo Gigy alimporomoshea Nandy kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy naye hakukaa kimya, na kuamua kumjibu Gigy kwa style yake, ambayo watu wameiona kama dharau kwa Gigy money. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy alipost video akihesabu hela kwenye UNGO NA KUANDIKA " Ukitaka vita na mpare, sogelea huo ungo ". Wadau wa mitandaoni wametoa maoni kuwa kitendo cha Nandy kupost hiyo video imeonekana ni kama 'Kijembe' kwa Gigy kuwa hana Muda wa kugombana na kujibu matusi yake, na badala yake yuko 'bize' kutafuta hela.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger