Ticker

6/recent/ticker-posts
.

‘Nilinunua Gari Langu na Pesa Zangu Bila ‘Top up,’Hamisa Amwambia Zari

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Hamisa Mobetto na mama wa mtoto wa staa wa bongo Diamond Platnumz amesema kuwa amelinunua gari lake na pesa zake mwenyewe na wala Diamond hakutoa hata shillingi wala kumuongezea pesa ili aweze kununua gari hilo.

Haya yanajiri baada ya Zari Hassan kusema kuwa Diamond alimuongezea pesa ili aweze kununua gari lake,  jambo ambalo liliibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii.


Hamisa amesema kuwa yeye si Zari kwa maana amejinunulia gari hilo peke yake.

“Nimetia bidii katika kazi yangu, kwa sasa sijapata usingizi kwa muda wa wiki tatu, kwa nakaa usingizi, nimenunua prado yangu na pesa zangu mwenyewe

Niliuza gari langu la kitambo na nikaongeza pesa zingine juu ili kununua prado, nilinunua na pesa zangu mwenyewe hamna mtu yeyote ambaye alichanga na kunisaidia kununua

Kama Diamond angenisaidia singekosa, kumshukuru.” Aliandika Hamisa.

Zari na Hamisa wamekuwa katika cheche za maneno kwenye mitandao ya kijamii huku Zari akidai kuwa Hamisa ni mchawi.


Kupitia kwenye mitandao ya kijamii, Mobetto aliposti video akiliendesha gari hilo na kuandika ujumbe mfupi

Post a Comment

0 Comments