7/29/2020

Rais wa BongoFleva D.Planet Ataja Watangazaji Wake Bora, B Dozen Hayupo


Rais wa BongoFleva Dullah Planet ambaye ni mtangazaji wa East Africa Radio na East Africa Tv ametaja orodha ya watangazaji 7 bora ambao  wanaofanya kazi nje na ndani ya Tanzania.Akitaja orodha hiyo kwenye show ya Chill na Sky, Dullah Planet aliambiwa ataje orodha ya watangazaji watatu bora anaowakubali ila kutokana na anaowakubali yeye ni zaidi ya hapo akaongeza wengine wanne ili kufikia 7.

"Napenda kazi ya kijana King Smash ambaye anafanya show ya The Cruise East Africa Radio, Captain Gadner G Habash anatangaza vizuri sana matamshi mazuri na Kiswahili nikimsikiliza nafurahi sana, Kuna dada anaitwa Zuhura Yunus ananyoosha sana Kiswahili, mwingine ni George Njogopa yupo vizuri mno, kaka Salim Kikeke anafanya kazi nzuri, kuna Raia wa Kenya anafanya kazi pale East Africa Radio anaitwa Ian Diallo ana voko ya hatari, wa mwisho ni Millard Ayo" amesema Dulla Planet
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger