Shilole Ageuziwa Kibao Kipigo cha Uchebe!


DAR: Sakata la staa wa filamu na Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kuchezea kipigo kutoka kwa mumewe, Ashraf Uchebe linazidi kuchukua sura mpya.

Kufuatia kusambaa kwa picha mpya zinazomuonesha mwanamama huyo akiwa hana kovu lolote wala dalili ya kupigwa, amegeuziwa kibao.

Mapema wiki hii, zilisambaa habari mitandaoni kwamba, Shilole na Uchebe wamerudiana hivyo gazeti hili lilizungumza na kila mmoja ambapo walikanusha kurudiana.

“Hapana, hakuna jambo kama hilo, hatujarudiana, tusubiri kwanza kwa sasa siwezi kuzungumzia jambo hilo,” amesema Uchebe.

Kwa upande wake, Shilole au Shishi Baby alitumia ukurasa wake wa Instagram kukanusha taarifa hizo akiwa jijini Arusha ambapo aliposti picha zikimuonesha akiwa mzima kabisa na ndipo raia wenye hasira kali walipomtolea uvivu;

“Ashitakiwe, hajapigwa, ilikuwa kutafuta kiki tu, yaani hana hata kovu…

“Shilole anatupa dhana ya kuamini kuwa mwanamke akitaka jambo lake, yupo tayari kutumia hata njia ya kishetani ili atimize lengo lake, Mungu atusamehe tuliomuhukumu Uchebe…

“Sijui wale mabingwa wa kurukia vitu wasivyokuwa na uhakika navyo kama Mwijaku wanajionaje sasa hivi? Ila inawezekana wanaona kama hakuna kilichotokea, namshauri Uchebe angembwaga mazima! Mwanamke akishafikia wakati wa kukufanyia hivi, huwa hakomi, anaweza kukusingizia chochote ilimradi tu uaibike…

“Shishi na Uchebe walikutania gereji kwa hiyo ni vigumu sana kuachana. Pia kama naona mimba kwa mbaaali (kwenye picha). Baba Levo ongeza sauti…

“Anaonekana hana kovu wala jeraha hata moja, kwa hiyo ilikuwa ni visa tu maana mwanamke akitaka kuachika hakosi visa…

“Picha za kipigo ni za zamani, halafu kipigo kipya hakupewa ila tu alitaka kuona namna Wabongo tulivyo wajinga wa kuwatetea wanawake warembo. Wanawake wangapi wanapigwa, halafu watu hawatoi povu?

“Nimegundua hakupigwa ila ni kutafuta kiki tu, kupigwa alipigwa zamani…

“Nimegundua kumbe ukipigwa, halafu uwe na pesa zako, mwenyewe unapona haraka…”

Ilisomeka sehemu ya maoni maelfu juu ya sakata la Shilole na kuonekana kwake akiwa hana kovu wala mkwaruzo.

Katika maelezo yake ya kukanusha kurudiana na Uchebe, Shilole alikuwa na haya ya kusema;

“Nimeona kuna taarifa nyingi zinatengenezwa, kuona uongo mwingi unapikwa kuhusu mimi na sakata la ndoa au kupigwa.

“Kuna video inasambazwa, tuko sisi na bwana mmoja anaitwa Aristote. Ile video ni ya siku nyingi sana. Naomba muipuuze.

“Suala langu lilihusisha vyombo vya dola au sheria. Hivyo siyo jambo la kusema tu kwa sasa. Wakati unakuja (siyo mbali), nitaeleza yote kwa utaratibu na kwa undani.”

Hivi karibuni Shilole aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram zikimuonesha akiwa na majeraha ya kupigwa akimtuhumu Uchebe kumshushia kipigo cha mbwa koko.

Hata hivyo, katika maelezo yake, Shilole alisema picha hizo ni za matukio tofauti bila kusema kama ni za hivi karibuni.

Katika utetezi wake baada ya kuona anashambuliwa kila kona hadi na viongozi serikalini, Uchebe alijitahidi kujitetea kwa kusema kwamba picha hizo ni matukio ya zamani na kwamba Shilole aliamua kuzitoa kufuatia kutofautiana naye baada ya kulala nje ya nyumbani kwake kwa siku mbili bila taarifa. That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments