8/19/2020

20 Percent: Siwezi Kuongelea Majina ya Wasanii Wanaofanya Vizuri Mpaka nao Waanze Kuniongelea MimiBaada ya kimya cha muda mrefu Mwanamuziki 20 Percent aliibukia na kutumbuiza katika tamasha la Chama cha Mapinduzi lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru siku ya Jumamosi. Katika tamasha hilo mwanamuziki huyu alionekana kukonga nyonyo za mashabiki na kupata shangwe la kutosha katika nyimbo zake hasa kutokana na msanii huyo kuja na Mama Neema, mwanamke ambaye aliigiza naye filamu pamoja na kumuimba wimbo maarufu uitwao "Mama Neema" .

Baada ya kumaliza kutumbuiza Mwanamuziki 20 Percent alipata nafasi ya kuhojiwa na Waandishi wa habari. Katika mahojiano hayo Mwanamuziki huyu alieleza mambo mbalimbali.

Alipoulizwa amejisikiaje baada ya kukaa kimya muda mrefu lakini aliporudi kutumbuiza aliweza kukonga nyoyo za watu na kushangiliwa sana 20 percent alisema kuwa jambo hilo linaonesha kuwa bado mashabiki wake wana upendo naye na bado anaishi mioyoni mwao.

Aidha, Walipomuuliza kuhusu suala la kurejea katika Muziki Mwanamziki 20 Percent alisema yeye bado anaendelea kufanya muziki m,uda wote labda kama wao ndio wameacha kumuona. Na pia, pamoja na kukaa kimya lakini bado watu wanampenda na hawajampotezea kwani bado wanaishi na nyimbo kama Mama Neema, Tamaa Mbaya na Yanini Malumbano. Ameongeza kuwa, kutokana na Shangwe alilopata katika tamasha hilo ameona kuna umuhimu wa kurejea tena katika muziki kwa sababu kukaa kimya pia ni muziki mzuri.

Wakihoji kuwa kutokana na mabadiliko ya muziki wa sasa akirejea atabadilika au ataendelea kufanya muziki wake wa zamani, 20 Percent ameahidi kurejea na kuleta muziki wa heshima na kukimbiza muziki wa matusi ambao umetawala kwa sasa. Amesema, "Watu wanavyoona 20 Percent narudi kwenye gemu wanajiandaa kuimba vizuri".

Aidha, wakihoji kuhusu kufanya muziki kuendana na soko la sasa, 20 Percent amesema Mimi silengi soko, nalenga fikra za mlalahoi na mtu yoyote ambaye huzuni yake ipo na hamna mtu wa kuiongelea.

Zaidi ya hayo, waandishi wa habari walipomtaka 20 Percent awataje wasanii wa sasa ambao anaona wanafanya vizuri alisema hawezi kuwataja wasanii hao mpaka pale watakapoanza kumuongelea yeye.

20 Percent amewashauri wasanii Kuacha kuimba kuhusu maisha yao binafsi na wajikite kuimba na kukuza fikra. amewataka wasanii waisaidie jamii kukuwa kifikra. Wawafanye mashabiki washabikie fikra zao na sio kuanza kushabikia maisha yao binafsi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger