8/09/2020

Alichokisema Haji Manara, Senzo Kwenda YangaBAADA ya Senzo Masingiza aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba kujiuzulu ndani ya klabu hiyo huku ikielezwa kuwa amepata kazi ndani ya Yanga uongozi wa Simba umesema kuwa Simba ni klabu kubwa.


 


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Haji Manara ameandika:” kwa hiyo mzunguko wa dunia umesimama siyo? Simba ni huge Club (klabu kubwa) our hope (matumaini yetu) kesho Senzo utakuja kukabidhi ofisi na nyaraka zetu kama utaratibu unavyosema. Kifuatacho.


Sababu kubwa inayotajwa kwa Senzo kubwaga manyanga ni kutokana na suala la usajili wa Bernard Morrison ambaye alitangazwa jana kuibukia ndani ya Simba akitokea Yanga.


Inaelezwa kuwa Morrison hakuwa chaguo la Senzo kusajiliwa kwake kumefanya akasirike na kujiweka pembeni.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger