COVID19 : Jamaa Aliyekataa Karantini Awaambukiza Wazazi, Wafariki Ghafla

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Aliwaambukiza wazazi wake ambao walifariki kutokana na ugonjwa huo yeye akisalia. Picha:Hisani

Waziri wa afya alibaini kuwa jamaa alifarki pamoja na mkewe baada ya kuambikzwa corona na mwanao

Mwanao huyo alipatikana na covid19 na kushauriwa kukaa karantini lakini akakataa

Kijana mmoja aliyepatikana na virusi vya corona sasa ameiangamiza famlia yake baada ya kukataa kufuata kanuni alizopewa.

Kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe, bwana huyo aliyepatikana na virusi hivyo alishauriwa kukaa karantini kwa muda hadi virusi vivyo vimtoke swala alilolipuuza na kuzidi kutangamana na familia yake.

Hatimaye aliwaambukiza wazazi wake ambao walifariki kutokana na ugonjwa huo yeye akisalia.

‘’ Nilipata habari kuwa kijana aliyepatikana na virusi vya corona na kukataa kukaa karantini akidai kuwa virusi hivyo havipo, alienda nyumbani, akawaambikiza wazazi wake na dadake. Kwa bahati mbaya baba na mama walifariki kwa ugonjwa huo,’’ Kagwe alisema kwa hasira.

Inadaiwa kuwa babake kijana huyo alifariki wiki moja tu baada ya mamake kufariki kutokana na virusi hivyo, wote wakithibitishwa kuugua maradhi mengine kabla kuambukizwa corona.

New coronavirus cases jump sharply in Europe, with Italy worst hit ...

Wahudumu wa afya wakijitayarisha kumzika aliyefariki na COVID19. Picha: Hisani

Waziri huyo alisisitiza kuwa atazidi kutangaza ripoti kuhusu maambukizi ya corona kila siku licha ya Wakenya  kulalamika kuhusu kuchoka na ripoti hizo.

‘’ Hatutakoma. Afadhali mchoke na idadi badala ya kuchoka kutazama paa za hospitali,’’ aliongezea.

Alisisitiza kuwa Wakenya lazima wafuata kanuni zilizotolewa na wizara ya afya katika kujikinga na virusi hivyo.

Haya yanajiri huku Tanzania ikishikilia kuwa vurusi hivyo vimepigwa teke humu nchini. Kulingana na Rais Magufuli, Watanzania wako huru kubanana maana corona haipo. Tanzania imekingwa na Mungu kutokana na virusi hivyo hatari.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad